|
Blogs |
|
|
 |
Apr 2nd, 2008 - 06:55:57 |
Terri
Siku iliyopita niliwaza na kuwazua juu ya walioathirika na kupoteza makao yao walivyojipata katika janga hili la ufukura usiooleweka hadi sasa! Mawazo haya yote yalinijia nikiwa nikishiriki misa kaninsani, na si ya kuwa misa hiyo ilikuwa si ya kufana la hasha, lakini mambo niliyoshuhudia yalinifanya kushikwa na ghababu kuu sana!
Tulipofika kanisani misa ilikuwa ishaanza na kwa hivyo hatukuwa na budi kujitetea kwa kwenda kujaribu kumshawishi mwalimu wa dini kutupa benchi moja ili tuweze kuitumia humo kanisani. Pengine bahati yetu kwasababu tuliweza kuwapata Vijana wavulana wawili waliotusaidia kubeba benchi ile. Mara tulipofika kanisani, kundi kubwa la watu lilivamia benchi hiyo na kukaa ikabidi mmoja wa Vijana hao kukosa hata nafasi ya kuweza kujisitiri! Lahaula, waliosema usistaajabu ya musa ya firauni hujayaona kweli alinena. Nilibaki mdomo wazi kwa vile sikuweza kufikiri ya kuwa jambo kama hilo lingeliweza kutendeka katika hadhara na kwa kusitiza hii iliyo na wakristo wanaomcha Mungu! Nilifunzwa tangu utotoni kumpa mtu yeyote haki yake na moja ya haki hizi kulingana name ni kumpa nafasi mtu aliyebeba benchi hiyo nafasi ya kwanza na ilkiwa itakuwa ipo bado basi wengine nao wafuate kuanzia wakubwazo!
Nilishangaa na kwa kuwa sikutaka kuonekana kuwa alipigwa na butwaa, mawazo mengi sana yalinijia na nikaweza kulinganisha yaliyotendeka na vile wahasiriwa waliopoteza makao yao yalivyonijia!
Jamani wenzangu twaweza kuishi maisha yasiokuwa na kuwanyang’anya wenzetu yaliyo yao ya haki??
Mar 20th, 2008 - 11:03:52 |
Terri
Ni vema kabisa kuelewa swala au mswaada wa mambo yanavyo endela nchini Kenya.Hivi tunavyozungumza, sheria mbili mwafaka za kuidhinisha ofisi ya Waziri mkuu na pia tume ya kuchunguza na kuhakikisha ukweli na haki zimeshatiwa sahihi na sasa zangojea tu kuandikishwa rasmi .
Twaona kwamba pia wanasiasa wameweza kuyaweka masilahi ya wakenya kwanza na kwa moyo wote kuunga mkono miswaada hii. Katika bunge, twaona ya kuwa Rais Kibaki alihudumu kikao hiki cha tatu kama Mbunge wa Othaya na wala si kama rais. Hii ni dhairi shairi kwamba pia yeye ameunga mikakati inayo endelea ya kuwezesha amani nchini Kenya. Chama cha ODM ambacho kilionekana kuweza kuanza kuwa na migogoro hivi karibuni , kupitia kwa msimamo ambao Kigogo wa Pentagon bwana Ruto aliokuwa ameuchukuwa, kimefikia maelewano ambayo yameleta utulivu. Bwana Ruto ametangaza hadharani kuwa anaunga mkono kuteuliwa kwa Bwana Musalia Mudavadi kama Naibu wa waziri mkuu. Bwana Ruto alitangaza haya akiwa katika eneo lake la bunge la allipohodhuria sherehe ya kuwatuza wanafunzi bora katika shule ya wanafunzi ya wasichna ya Eldoret.Musalia Mudavadi anayejulikana kwa umaarfufu kama ‘Double M’ , ni mbunge wa Sabatia katika mkoa wa Magharibi.
Twaomba kama wakenya na hasa wana TIG ya kuwa miswaada iliyoutiwa sahihi, itafuata kwa makini na kila anayehusika atatia for a na kufanya jukumu lake la kuhakikisha ya kuwa mambo yaliyojadiliwa yatatimizwa.
Page:
1
(Total Blogs: 2)
feed
|
 |
 |
 |
|